1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bottas aipa Mercedes taji lake la sita

14 Oktoba 2019

Lewis Hamilton anaweza kusonga hatua moja karibu na rekodi ya Michael Schumacher ya mataji saba ya ulimwengu, wakati mashindano hayo yatahamia Mexico katika wiki mbili zijazo

https://p.dw.com/p/3RGWY
Sport Formel 1 - Großer Preis von Japan l Jubel Valtteri Bottas
Picha: Reuters/I. Kato

Wikiendi iliyokuwa ikionekana nzuri kwa timu ya Ferrari ilikamilika kwa Mercedes kuwa timu ya kwanza kutwaa mataji ya sita mfululizo ya dereva bora na kampuni bora. Sasa swali tu ni dereva yupi wa Mercedes atakayenyakua taji la dereva bingwa duniani.

Ijapokuwa Valtteri Bottas alipata ushindi wake wa tatu msimu huu katika mashindano ya Grand Prix ya Japan jana jumapili, nafasi ya tatu aliyomaliza mwenzake Hamilton nyuma ya Sebastian Vettel wa Ferrari ina maana taji lake la sita la ubingwa wa dunia lipo mikononi mwake. "Kwanza, ni pongezi kwa timu yangu, ilistahili kushinda taji hili kwa miaka sita mfululizo, taji la kampuni bora ya kutengeneza magari, hicho ndio cha msingi. Nilitaka tu kukusanya pointi kwa ajili ya timu leo". Alisema Hamilton

Hamilton anaongoza orodha ya madereva na mwanya wa pointi 64 dhidi ya Bottas. Kuna mashindano manne yaliyobaki kwa msimu kukamilika.