1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Boris Johnson asema alilipotosha Bunge kuhusu 'partygate'

22 Machi 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson amekiri kuwa alitoa habari za uwongo kwa Bunge kuhusu sherehe za serikali ambazo ziliandaliwa kwa kukiuka vizuizi vya maambukizi ya UVIKO-19.

https://p.dw.com/p/4P31Y
England London | Boris Johnson
Picha: Kin Cheung/AP/picture alliance

Hata hivyo Boris Johnson amesisitiza kuwa hakulipotosha kwa makusudi Bunge kuhusu hafla hizo.

Waziri mkuu huyo wa zamani alitoa kauli hizo kabla ya kuhojiwa na kamati ya bunge katika kikao kinachopangwa leo mchana.

Katika ushahidi wake ulioandikwa kwa Kamati hiyo ya Bunge, Johnson alisema kuwa taarifa alizotoa kwa bunge kuwa sheria zilifuatwa wakati wote mwishowe hazikuwa sahihi.

Alidai kuwa taarifa zake zilifanywa kwa nia njema na kwa misingi ya kile alichokijua na kukiamini kwa wakati huo.

Boris alijiuzulu wadhifa wa waziri mkuu mwaka wa 2022 kufuatia kashfa kadhaa, zikiwemo ripoti kuwa yeye na wafanyakazi wa serikali waliandaa mikusanyiko iliyokiuka sheria za UVIKO-19.