Boni Yayi mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika
29 Januari 2012Viongozi wa Umoja wa Afrika wanaokutana kwa siku mbili mjini Addis Ababa Ethiopia pia hii leo wanatarajiwa kumchagua mkuu wa baraza la amani na usalama wa Umoja wa Afrika kuchukua nafasi ya Jean Ping kutoka Gabon.
Ping anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa waziri wa jamii wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma. Afrika kusini imesema inaamini Nkosazana Zuma aliyekuwa mke wa rais Jacob Zuma ana nafasi kubwa ya kuchukua kiti hicho kutoka kwa Ping aliyeteuliwa mwaka wa 2008.
Mkutano huo wa kilele unafanyika katika makao makuu mapya ya umoja huo yaliojengwa na China mjini Adis Ababa. Kati ya maswala yatakayojadiliwa ni kuimarishwa bishara Afrika, mzozo wa Somalia na pia mzozo wa mafuta kati ya Sudan na Suda kusini.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon anaehudhuria mkutano huo amewatolea mwito viongozi wa Afrika waheshimu haki za mashoga.