1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 9 wauwawa kwa bomu la kutegwa ardhini Syria

10 Aprili 2023

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu nchini Syria limesema watu tisa waliokuwa wakitafuta chakula wameuawa baada ya gari waliyokuwemo kukanyaga bomu lililotegwa ardhini kaskazini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4Ps6O
Syrien | Explosion durch Landmine in Syrien
Picha: LOUAI BESHARA/AFP

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu nchini Syria limesema watu tisa waliokuwa wakitafuta chakula wameuawa baada ya gari waliyokuwemo kukanyaga bomu lililotegwa ardhini kaskazini mwa nchi hiyo.

Kufuatia mkasa huo ulitokea katika jimbo la Deir al-Zour, watu wengine watatu wamejeruhiwa.

Shirika hilo la uangalizi linasema watu wanaosaka chakula kama sehemu ya kujikimu kimaisha nchini Syiria wapo hatarini kwa mabomu ya ardhini pamoja na mashambulizi ya kundi lijiitalo Dola la Kiislamu.

Rekodi zinanonesha tangu mwanzoni mwa Januari mwaka huu, jumla ya Wasyria 137 wameuwawa katika miripuko ya mabomu ya ardhini wakiwemo watoto 30.