Bolsonaro kukata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama
1 Julai 2023Matangazo
Uamuazi huo uliotolewa jana unatokana na matamshi ya Bolsonaro ya mwaka 2022 alipoukosoa mfumo wa upigaji kura wa nchi hiyo bila kutoa ushahidi.
Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia amewaambia waandishi habari kwamba uamuzi wa mahakama ni "usaliti" na anajitayarisha kukata rufaa kwenye mahakama kuu.
Hukumu hiyo ya mahakama inaamanisha Bolsonaro hataruhusiwa kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2026.
Alipelekwa mahakamani na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kwa kutoa madai bila ushahidi kwamba, mfumo wa upigaji kura kwa njia ya elektroniki unaotumika nchini Brazil tangu mwaka 1996 umevuruga uwazi kwenye uchaguzi.