1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Blinken: nafasi sawa za kibiashara kati ya China na Marekani

25 Aprili 2024

Antony Blinken ametoa wito kwa China kutoa nafasi sawa kwa biashara za Marekani wakati alipoanza ziara inayolenga kutatua masuala tete baina ya Washington na Beijing.

https://p.dw.com/p/4fBh7
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken awasili Beijing China
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken awasili Beijing ChinaPicha: Mark Schiefelbein/AP//Pool AP/dpa/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Matthew Miller, amesema kuwa wakati wa mkutano na afisa mkuu wa China mjini Shanghai Chen Jining, Blinken alielezea wasiwasi kuhusu sera za kibiashara za China na taratibu za kiuchumi zisizokuwa za kisoko.

Blinken pia alisisitiza kuwa Marekani inatafuta ushindani mzuri wa kiuchumi na China na nafasi sawa kwa wafanyikazi wake na kampuni zake nchini humo.

Akiwa Shanghai, Blinken pia alifanya mazungumzo na viongozi wa kibiashara pamoja na wanafunzi wa Marekani na China wa tawi la chuko kikuu cha New York nchini humo ambapo alisema kuwa muingiliano wa kitamaduni ni njia sahihi ya kuhakikisha kuwa wanaanza kwa matumaini ya kuelewana.