1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken na Baerbock wajadili mshikamano na kuisaidia Ukraine

16 Septemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock wamefanya mazungumzo na kutilia mkazo mshikamano na ushirika wao.

https://p.dw.com/p/4WPuk
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock walipokutana mjini Washington Picha: Thomas Koehler/photothek/picture alliance

Kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Washington jana Ijumaa mawaziri hao walivizungumzia pia vita vya Ukraine ambapo Baerbock amesema vinazidi kuimarisha shauku ya  taifa hilo kupigania uhuru na kutengwa kimataifa kwa rais Vladimir Putin wa Urusi.

Baerbock amesema mazungumzo yake na Blinken yaligusia pia namna kuunganisha msaada wa pamoja wa nchi zao kwa Ukraine wakati wa msimu wa baridi unaokaribia.

Katika hatua nyingine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ataitembelea Marekani wiki ijayo kwa mara ya pili, tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini mwake.

Hayo yameelezwa na ikulu ya Marekani ambayo imesema  Zelensky, atakutana na Rais Joe Biden kwa mazungumzo ya kuirai Marekani kuendelea kuisaidia nchi yake iliyo vitani.