SiasaMarekani
Blinken: Mazungumzo yaweza kuwa fursa ya mwisho kwa Gaza
19 Agosti 2024Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema hivi Jumatatu kwamba mazungumzo yanayotarajiwa kuanza wiki hii nchini Misri, yanaweza kuwa "fursa ya mwisho" ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.
Blinken ambaye yuko ziarani mjini Tel-Aviv, ikiwa ni ziara yake ya tisa tangu shambulizi la Oktoba 7, amekutana Jumatatu asubuhi na Rais wa Israel Isaac Herzog kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Marekani, Misri na Qatar wamekuwa wapatanishi katika mfululizo wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Israel na kundi la Hamas.
Duru za hivi punde za mazungumzo ya siku mbili nchini Qatar zilimalizika bila mafanikio makubwa siku ya Ijumaa.