1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken kufanya ziara nyingine Mashariki ya Kati

Josephat Charo
4 Januari 2024

Ziara hiyo inafanyika wakati hofu ikiongezeka kwamba vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza vitasambaa katika eneo zima kufuatia milipiko ya mabomu nchini Iran na kuuliwa kwa kiongozi wa Hamas nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4aqu4
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ametarajiwa kuanza ziara huko Mashariki ya Kati
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ametarajiwa kuanza ziara huko Mashariki ya KatiPicha: Saul Loeb/Pool/AFP

Afisa wa Marekani ambaye hakutaka kutambulishwa amethibitisha ziara ya Blinken ambayo ni ya nne Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Afisa huyo hakutoa taarifa za kina kuhusu ziara ya Blinken mbali na kusema itajumuisha Israel.

Tangazo la ziara ya Blinken limetolewa baada ya watu 95 kuuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa nchini Iran katika milipuko miwili iliyotokea wakati mmoja karibu na kaburi la jenerali wa jeshi la mapinduzi la Iran aliyeuwawa, Qasem Soleimani.

Iran imeinyooshea kidole cha lawama Marekani na Israel kwa shambulizi hilo. Marekani imeyakataa madai hayo yanayopendekeza kuhusika kwa nchi hizo mbili.