Blinken atua Israel katika juhudi za kutatua vita vya Gaza
22 Machi 2024Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, amewasili mjini Tel Aviv nchini Israel leo, kituo cha mwisho cha ziara yake ya sita katika eneo la Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza.
Blinkenamesema kuwa atapendekeza njia mbadala kuhusu mashambulizi ya ardhini yaliopangwa na Israel katika mji wa Rafah ulioko Kusini mwa Gaza atakapokutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na baraza lake la mawaziri la vita.
Hapo jana, Blinken na viongozi wa mataifa ya Kiarabu, walijadili kuhusu juhudi za kusitisha mapigano na hatima ya Gaza ya baada ya vita.
Haya yanajiri wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura leo kuhusu azimio lililowasilishwa na Marekani la kutangaza umuhimu wa kusitishwa mara moja kwa vita hivyo vya Gaza.