Blinken atarajiwa wiki ijayo kufanya ziara barani Ulaya
28 Machi 2024Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller amesema kuwa Blinken ataelekea mjini Paris na kukutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kujadili kuhusu msaada kwa Ukraine, juhudi za kuzuia kuongezeka kwa mzozo wa Gaza, na masuala mengine muhimu.
Baadaye Aprili mosi hadi tano, Blinken ataelekea mjini Brussels nchini Ubelgiji ili kudhihirisha jukumu la Marekani katika Jumuiya ya Kujihami NATO, kuimarisha ushirikiano na kujadili namna ya kushughulikia changamoto za kimataifa.
Mnamo Aprili 4, Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO watajumuika katika sherehe za kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya kujihami ya NATO. Blinken atalitembela pia jiji la Ubelgiji la Leuven, ambapo atahudhuria mkutano wa Baraza la Biashara na Teknolojia la Umoja wa Ulaya na Marekani.