Blinken ataka msimamo wa G7 kuhusu vita vya Israel na Hamas
7 Novemba 2023Blinken ameutoa wito huo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa mambo ya nje wa Kundi la mataifa ya Magharibi yaliyoendelea kiviwanda G7 huko nchini Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa ameelezea vipengee muhimu vitakavyojadiliwa kuhusu mzozo huo wa Mashariki ya Kati:
"Kuhusu hali ya dharura huko Palestina na Israel, tulisisitiza dhamira yetu ya kuachiliwa mara moja kwa mateka, kuhakikisha usalama wa raia, uheshimishwaji wa sheria za kimataifa kwa pande zote zinazohusika, kuwepo utulivu wa haraka katika mzozo huu, kuboresha hali ya kibinadamu na kutoa wito wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kiutu," alisema Kamikawa.
Mawaziri hao wa mahusiano ya kigeni wa G7 wanatarajia pia kujadili uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, suala la mahusiano na Asia ya Kati yenye utajiri wa rasilimali, lakini pia ushawishi wa China unaozidi kuimarika duniani.