1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Blinken: Urusi ilipokea makombora kutoka Iran

10 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amedai hii leo kuwa Urusi ilipokea makombora ya masafa marefu kutoka Iran ambayo huenda yakatumiwa dhidi ya Ukraine katika wiki chache zijazo.

https://p.dw.com/p/4kTVy
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Uingereza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy kwenye mkutano na waandishi wa habari.Picha: Mark Schiefelbein via REUTERS

Blinken ameyasema hayo London kabla ya ziara yake Kyiv ambako ataambatana na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy.

Waziri huyo ameonya kwamba ushirikiano kati ya Moscow na Tehran unatishia usalama mpana wa Ulaya.

Blinken alisema "Putin pia anategemea zaidi usaidizi kutoka kwa Iran na Jamhuri ya watu wa Korea Kaskazini katika matukio haya, kupata silaha kinyume na maazimio mengi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."

Washington ilikuwa imeionya Iran kwamba kuipatia Urusi makombora ya masafa marefu kunaweza kuzidisha mvutano na vikwazo vipya.