Blinken asema Israel inahitaji kuisaidia Palestina
17 Januari 2024Blinken amerudia wito wake wa kuwepo "njia ya kuelekea kupatikana kwa taifa la Palestina" licha ya Marekani kuiunga mkono Israel katika vita vyake dhidi ya kundi la Hamas.
Mwanadiplomasia huyo wa Marekani ameongeza kuwa, mamlaka ya Palestina inaweza tu kuwa na ufanisi iwapo itafanya kazi kwa ushirikiano wa Israel na wala sio upinzani.
"Unazungumza juu ya utawala, serikali na muundo wa utawala, ambao utaiwezesha mamlaka ya Palestina kuwapa mahitaji raia wa Palestina. Kwa hivyo, mamlaka hiyo inapaswa iwe inafanya kazi katika mazingira mazuri, kwa maneno mengine, isaidiwe na Israel na wala sio kukabiliwa na upinzani, alisema Blinken"
Msaada zaidi wa kibinaadamu kuwasili Gaza
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa muda mrefu ameonyesha upinzani kwa mamlaka ya Palestina na uwepo wa taifa huru la Palestina.