1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken afanya mazungumzo na viongozi wa Poland

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na viongozi wa Poland ambayo ni mshirika mkuu, juu ya njia za kuiunga mkono Ukrainne, huku mashambulizi ya Urusi na uchaguzi Marekani vikiibua hofu.

https://p.dw.com/p/4kYmL
aziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
aziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Roberto Schmidt/Pool photo via AP/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani alifanya mazungumzo na uongozi wa Poland mjini Warsaw baada ziara yake nchini Ukraine.

Soma pia:Guterres: Kitisho kwa usalama wa dunia kikubwa zaidi sasa

Blinken ameahidi kupitia kwa haraka ombi la Ukraine la kupatiwa kibali cha kuzitumia silaha za Magharibi ndani ya ardhi ya Moscow. Blinken amekutana kando mjini Warsaw na Waziri Mkuu Donald Tusk na Rais Andrzej Duda, ambao ni wapinzani wakubwa juu ya mwelekeo wa mwanachama huyo wa Umoja wa Ulaya.