1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Lazima tusimame pamoja dhidi ya Urusi

Josephat Charo
26 Juni 2022

Rais wa Marekani Joe Biden amesifu umoja wa jumuiya ya kimataifa unaoendelea kushuhudiwa katika kuikabili Urusi. Biden aliyasema hayo wakati yeye pamoja na viongozi wa nchi zilizostawi zaidi kiviwanda duniani G7

https://p.dw.com/p/4DGxs
Deutschland I G7-Gipfel auf Schloss Elmau in Garmisch-Partenkirchen
Picha: IMAGO

Biden na wenzake walikutana kujadili jinsi ya kuhakikisha wanapata vyanzo vya uhakika vya nishati na kulitafutia ufumbuzi jinamizi la mfumuko wa bei, kwa lengo la kuepusha athari zinazotokana na vita kusababiswha mpasuko katika muungano wa dunia unaofanya kazi kwa bidii kidhibu serikali ya mjini Moscow. Viongozi hao walitarajiwa kutangaza marufuku mpya ya uagizaji wa dhahabu ya Urusi, hatua mpya katiak mkururuo wa vikwazo ambavyo kundi hilo la nchi zilistawi kidemokrasia zinatumai itaitenga zaidi Urusi kiuchumi kutokana na uvamizi wake wa Ukraine.

Viongozi wameungana pamoja katika ubia mpya wa ushirikiano katika suala la miundombinu unaonuiwa kutoa uwekezaji mbadala kwa ule wa Urusi na China katika nchi zinazoendelea. "Lazima tuhakikishe tubaki pamoja," alisema rais Biden wakati wa kikao chake na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, kabla kuanza kwa mkutano wa G7. Ujerumani inashikilia urais wa kupokezana wa nchi za kundi la G7 na inauandaa mkutano wa mwaka huu huku Emmau katika jimbo la kusini la Bavaria.

"Unajua, nitaendelea kushughulikai changamoto za kiuchumi zinazotukabili lakini nadhani tushikamane pamoja katika hili," aliongeza kusema Biden.

G7 Gipfeltreffen Schloss Elmau
Kutoka kushoto, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais wa Marekani Joe Buiden na Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris JohnsonPicha: Leonhard Foeger/REUTERS

Scholz alijibu akisema "ujumbe mzuri" ni kwamba "tumefanikiwa kushikamana pamoja, jambo ambalo Putin hakulitarajia," akimzungumzia rais wa Urusi Vladimir Putin, abmaye aliyatuma majeshi yake kuvuka mpaka na kuingia Ukraine mwishoni mwa mwezi wa Februari.

"Lazima tubaki pamoja, kwa sababu Putin amekuwa akitegemea tangu mwanzo, kwamba kwa njia fulani jumuiya ya kujihami NATO na nchi za G7 zitagawanyika, lakini hatujafanya hivyo na hatutagawanyika," alijibu Biden, wakati yeye na Scholz walipokaa kwa mazungumzo.

"Hatuwezi kuruhusu uchokozi huu uchukue taswira iliyonayo na tusichukue hatua," aliongeza Biden.

Saa kadhaa kabla mkutano kufunguliwa rasmi Urusi ilianzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya mji mkuu Kyiv siku ya Jumapili na kuyalenga majengo angalu mawili ya makazi ya raia, alisema meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko. Yalikuwa mashambulizi ya kwanza ya aina hiyo kuwahi kufanyw ana Urusi katika kipindi cha wiki tatu.

Chanzo: AP