Biden kutohudhuria Mkutano wa kilele wa COP28
27 Novemba 2023Wajumbe takriban 70,000 wakiwemo viongozi wa nchi pamoja na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wa COP28 utakaofunguliwa alhamisi ambao huenda ukawa ndio mkutano wa kilele mkubwa zaidi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira kuwahi kufanyika.
Soma pia: Wataalam wa Afya: Watetezi wa nishati ya visukuku wasishiriki COP28
Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu sababu za Rais Biden kutohudhuria COP28. Kwa mujibu wa afisa mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, serikali ya Biden bado iko kwenye majadiliano kuhusu ikiwa itatuma afisa wake wa ngazi ya juu kwenye mazungumzo hayo ya Dubai.
Mjumbe anayehusika na mazingira nchini Marekani na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje John Kerry ataongoza mashauriano ya kila siku kwa niaba ya nchi hiyo.