Biden kuitembelea Afrika katikati ya Oktoba
30 Septemba 2024Biden ameichagua Angola kama nchi ya ya kwanza katika safari yake barani Afrika kama rais, uamuzi unaoonesha ushawishi wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwa Marekani.
Angola ni mojawapo ya malengo ya miradi mikubwa ya miundombinu ya Marekani barani Afrika katika juhudi zake za kukabiliana na uwekezaji wa China.
Soma zaidi: Biden kuyatembelea maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Helene
Ziara hiyo ya Biden itakayoanza Oktoba 13 hadi 15 ataifanya ikiwa imebaki miezi michache tu kabla ya muhula wake kumalizika.
Yatakayozingatiwa kwenye ziara hiyo ni pamoja na mradi mkubwa wa kimataifa wa kukarabati reli yenye urefu wa kilomita 1,300 ambayo itaunganisha nchi za bara la Afrika zenye utajiri wa madini na bandari ya Angola ya Lobito iliyoko kwenye Bahari ya Atlantiki.