1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Biden awatunuku medali ya Uhuru kwa Messi,na wengineo

5 Januari 2025

Rais Joe Biden wa Marekani amewatunuku Nishani ya Rais ya Uhuru watu 19 mashuhuri akiwemo nguli wa soka duniani Lionel Messi na mwigizaji maarufu Denzel washington ikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuondoka madarakani

https://p.dw.com/p/4opbr
Marekani| Biden
Mwigizaji Denzel Washington akitunukiwa Nishani ya Uhuru na Rais Joe Biden katika ikulu ya MarekaniPicha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Rais Joe Biden wa Marekani amewatunuku Nishani ya Rais ya Uhuru watu 19 mashuhuri akiwemo nguli wa soka duniani Lionel Messi na mwigizaji maarufu Denzel washington ikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuondoka madarakani. 

Wakati wa hafla hiyo katika Ikulu ya Marekani, rais huyo anayemaliza muda wake aliwasilisha nishani hiyo ya heshima ya juu zaidi ya kiraia nchini Marekani kwa watu hao mashuhuri duniani. Nguli wa mpira wa vikapu Earvin "Magic" Johnson, mbunifu wa mitindo Ralph Lauren, na mwingizaji Michael J Fox, na mwanamuziki wa Rock Bono ni miongoni mwa wengine waliotunukiwa nishani hiyo.

Soma zaidi.Marekani yapanga kuiuzia Israel silaha za dola bilioni 8 

Taarifa ya Ikulu ya Marekani ya White House imesema tuzo hiyo ya kifahari hutolewa kwa watu ambao juhudi zao zimetoa mchango mkubwa kwa ustawi wa jamii,maadili, usalama wa Marekani, amani ya dunia, au jamii nyingine muhimu.

Tukio hilo limefanyika siku chache kabla ya Biden kukabidhi ofisi kwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump mnamo Januari 20.