1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden akosoa sheria ya Uganda dhidi ya mashoga

30 Mei 2023

Rais wa Joe Biden wa Marekani ameikosoa sheria mpya ya Uganda dhidi ya mapenzi ya jinsia moja akisema ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, na kutishia kupunguza misaada na uwekezaji katika nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4RyEP
Homosexuellenrechte in den USA
Picha: Sarah Silbiger/REUTERS

Alitoa wito wa kufutwa mara moja kwa hatua hizo mpya na kali, ambazo zinaeleza kwamba miongoni mwa mambo mengine kujihusisha na vitendo vya ushoga nchini Uganda litakuwa ni kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha maisha.

Soma pia: Museveni asaini sheria ya mapenzi ya jinsia moja

Akijiunga na msururu wa watu wanaomkosoa Rais Yoweri Museveni baada ya kusaini mswada wa sheria hiyo kuwa sheria kamili, Rais Biden amekiita kuwa kitendo cha kuruhusu matumizi ya sheria hiyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wote.