1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden ahutubia hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa

22 Septemba 2021

Rais Joe Biden wa Marekani ameitaka dunia kuongeza nguvu katika kukabiliana na janga la Covid-19, mabadiliko ya tabia nchi na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

https://p.dw.com/p/40dVH
New York UN Vollversammlung | Rede Präsident Joe Biden
Picha: EDUARDO MUNOZ/REUTERS

Katika hotuba yake ya kwanza ya ufunguzi,Joe Biden amezungumzia migogoro ya kijeshi na kuongeza pia, Marekani haitafuti vita mpya baridi na hasimu wake wa kibiashara China.

Wakati akiwasisitiza viongozi wenzake umhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano, Biden ameonekana kukwepa kujibu ukosoaji kutoka kwa washirika wake juu ya namna tata ya Marekani ilivyojiondoa Afghanistan na tofauti za sasa kidiplomsia na Ufaransa.

Lakini badala yake alitumia jukwaa hilo la kila mwaka kusema Marekani itaendelea kuwa mshirika wa kutegemewa wa kimataifa baada ya kile alichokisema sera ya mambo ya nje ya mtangulizi wake, Donald Trump ya Marekani kwanza. Kuhusu makabiliano ya mabadiliko ya tabia nchi Biden ametoa ahadi ya msaada wa mataifa masikini wa dola bilioni 11.4 kwa mwaka."Mwezi Aprili nilitangaza kwamba Marekani itaongeza mara mbili msaada wetu wa kifedha, katika kusaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na janga la kimazingira na leo najivunia kutangaza, tutatafanya kazi na bunge la Marekani, kuongeza idadi hiyo mara mbili tena, zikiwemo juhudi za kukabiliana." alisema kiongozi huyo.

Fuko na makibiliaoni ya kadhia ya tabia nchi lina upungufu wa dola biloni 20

New York UN Vollversammlung | Rede Präsident Joe Biden
Rais Biden akihutubia viongozi wa mataifaPicha: EDUARDO MUNOZ/REUTERS

Ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa zingato la makubalino ya Paris, jumuiya ya kimataifa ilipanga kukusanya kiasi cha dola bilioni 100 kwa mwaka katika kufanikisha jitihada hiyo, jambo ambalo hata hivyo halikufikiwa lengo. Utafiti mpya unaonesha kumekuwepo na upngufu wa dola bilioni 20 na sasa katika ahadi yake mpya Biden anasema itasiadia mataifa masikini kufikia malengo yao.

Aidha amezungumzia haki za binaadamu kwa kusema Marekani itandelea kuwa madhubuti kusimamia suiala hilo na halitazifumbia macho nguvu za kisiasa kwenda kinyume na jambo hilo. Kuhusu janga la Covid 19 amesema wasiwasi mkubwa wa kidunia kwa wakati huu hauwezi kutatuliwa kwa nguvu za kijeshi, aina mpya ya virusi hawezi kuangamizwa kwa bomu au mtutu wa bunduki, badala yake uongozi wa dunia kufanya kazi kwa pamoja.

Marekani ipo tayari kurejea katika makubaliano ya mpango ya nyuklia wa Iran

Kuhusu mzozo wa nishati ya nyuklia wa Iran amesema, Marekani bado ipo katika wajibu wake wa kuizuia Iran isitengeneze silaha za nyuklia. Wako tayari kuihusisha Iran katika suluhu ya kidiplomasia na wako tayari kurejea kwa ukamilifu katika kile kinachojulikana kama Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), wa unaosimamia makubaliano ya nyuklia ya 2015, endapo Iran pia itakuwa na utayari huo.

Kadhalika, amegusia suala la kuondosha nguvu ya matumizi ya silaha za nyuklia ya katika rasi ya Korea, na kwa hilo amesema kuna hatua madhubuti zimefikiwa ambazo zinaongeza hali ya utulivu katika eneo hilo.

Chanzo: APE