Biden aboronga wakati Trump akitoa uongo mdahalo wa urais
30 Juni 2024Juu ya yote, washirika wa Joe Biden walimtaka kuonyesha uthabiti na nguvu kwenyejukwaa la mdahalo jana usiku, ili kusaidia kutuliza maswali kuhusu uwezo wa kimwili na kiakili wa mdemokrati huyo mwenye umri wa miaka 81.
Lakini kwenye jukwaa kubwa zaidi la siasa za Marekani, Biden hakukidhi hata matarajio yao ya wastani.
Na hadi kufikia mwisho wa mpambano huo wa dakika 90, washirika wa Rais huyo, wakiwemo wapanga mikakati wa chama sawa na wapigakura, walikuwa wamejawa na hofu kubwa kutokana na utendaji wake, ambao ulikumbwa na kujikwaa kwa mara kwa mara, kusisita katika maelezo yake na mtindo wa kuongea kwa utulivu, ambao mara nyingi ilikuwa vigumu kumuelewa.
Soma zaidi: Biden, Trump wakabiliana katika madahalo wa kwanza wa uchaguzi wa rais 2024
Hadharani na kwa faragha, Wanademokrat walihoji iwapo chama kinaweza au kinapaswa kumbadilisha kama mgombeaji wa urais wa chama dhidi ya Rais wa zamani Donald Trump mwenye umri wa miaka 78 kwenye uchaguzi baadae mwaka huu.
"Siyo mimi pekee ambaye moyo wake unavunjika kwa sasa. Kuna watu wengi ambao walitazama mdahalo huu usiku wa leo na walihisi vibaya sana kwa Joe Biden," Seneta wa zamani wa Democratic Claire McCaskill alisema kwenye kituo cha MSNBC. "Sijui ikiwa kuna mambo yanaweza kufanyika kurekebisha hii."
Kwa sasa, swali kubwa kwa Biden ni ikiwa uharibifu huo ni wa kudumu. Wapiga kura wengi bado hawajajihusisha na uchaguzi huu ambao bado umebakiza zaidi ya miezi minne. Rais na washirika wake bado wamekalia mamilioni ya dola ambazo bado hazijatumika kwenye matangazo na na miundombinu ya majimbo ya maamuzi.
Fuatilia: Biden, Trump watofautiana vikali kuhusu rekodi zao katika mdahalo
Na kuna kielelezo cha kuimarika kutokana na utendaji mbaya katika midahalo, ikiwa ni pamoja na kurejea kwa Barack Obama baada ya kukutana na Mitt Romney mwaka wa 2012. Mdemokrat John Fetterman aliendelea kumshinda mpinzani wake wa chama cha Republican mwaka wa 2022 baada ya kuhangaika katika mjadala miezi kadhaa baada ya kukumbwa na kiharusi.
Kamari ya Biden
Kampeni ya Biden ya kuchaguliwa tena 2024 imekuwa ikiendeshwa kwa msingi kwamba wapiga kura hatimaye watamuunga mkono mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umaarufu ulioporomoka katika mchuano wa marudiano ambao Wamarekani wachache wanautaka.
Licha ya udhaifu kama huo, timu ya Biden ilisisitiza kwamba alikuwa na nafasi ya kipekee ya kumzuia Trump kurudi White House, kama alivyofanya miaka minne iliyopita.
Kwa muda mrefu wametabiri kwamba muungano wa ushindi wa kisiasa wa Biden hatimaye utamkumbatia rais huyo mdemokrat, baada ya kukumbushwa vya kutosha juu ya uongozi wa machafuko wa Trump. Lakini kulikuwa na dalili ndogo za imani kama hiyo kufuatia utendaji duni wa Biden katika mdahalo huo.
"Ulikuwa ni mwanzo wa polepole. Hilo liko wazi kwa kila mtu. Sitajadili suala hilo," Makamu wa Rais Kamala Harris alisema kwenye CNN baada ya mjadala huo. "Ninazungumzia uchaguzi wa Novemba. Ninazungumzia moja ya chaguzi muhimu zaidi katika maisha yetu ya pamoja."Mamilioni ya Wamarekani kufuatilia mdahalo wa Televisheni kati ya Joe Biden na Donald Trump
Wasaidizi wa Biden walichelewa kuingia kwenye chumba cha kuzungumza na waandishi habari baada ya mdahalo huo uliofanyika Atlanta. Na hatimaye walipoibuka, kwa kiasi kikubwa waliepuka maswali kutoka kwa waandishi wa habari. Badala yake, walikosoa orodha ndefu ya uwongo ya Trump wakati wa mjadala. Miongoni mwa mambo mengine, Trump hakujitenga na walioshambulia Bunge mnamo Januari 6, 2021.
Gavana wa California Gavin Newsom, amabye anatazamiwa kuwa mgombea urais wa baadaye na alikuwa mtetezi mashuhuri zaidi wa Biden katika chumba cha habari mjini Atlanta, aliwataka Wanademokrasia wasiwe na hofu.
"Nadhani haisaidii. Na nadhani haina ullazima. Lazima tuingie, tunapaswa kuinua vichwa vyetu," Newsom ilisema katika mahojiano na MSNBC. "Lazima tumunge mkono rais huyu. Huwezi kukata tamaa kwa sababu ya matokeo mabaya ya mdahalo mmoja. Ni chama cha aina gani kinafanya hivyo?"
Dalili za wasiwasi
Bado, dalili za wasiwasi zilionekana wazi baada ya Wademokrat kuanza kukihimiza chama wazi wazi kitafuta mgombea mbadala kwa Biden. Baadhi ya maafisa wa chama walionyesha chapisho la mtandao wa kijamii kutoka kwa aliyekuwa msaidizi wa kampeni ya Obama, Ravi Gupta.
"Kila Mdemokrat ninayemfahamu anatuma ujumbe mfupi wa maandishi kwamba hii ni mbaya," Gupta aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Sema tu hadharani na uanze kazi ngumu ya kuunda nafasi katika mkutano wa mchakato wa uteuzi. Nitapigia kura maiti badala ya Trump, lakini hii ni misheni kujitoa muhanga."
Chini ya sheria za sasa za Chama cha Democratic, itakuwa vigumu, kama siyo kutowezekana kabisaa, kuchukua nafasi ya Biden kama mteule wa chama bila ushirikiano wake au bila maafisa wa chama kuwa tayari kubadili sheria zake katika mkutano mkuu wa taifa wa Agosti.
Rais Biden alishinda idadi kubwa ya wajumbe wa Democratic wakati wa mchakato wa mchujo wa jimbo kwa jimbo. Na kanuni za chama zinasema kwamba, "wajumbe waliochaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kitaifa kwa ajili ya mgombea urais wataonyesha kwa dhamiri njema hisia za wale waliowachagua."Biden na Trump waendelea kujipigia debe
Lakini sheria za DNC hazina kanuni kali za "mjumbe asiye mwaminifu" kama ilivyo kwa mkutano wa chama cha Republican, RNC, ambao unapuuza kura dhidi ya ukiukaji wa msimamo ulioahidiwa na mjumbe.
Warepublican, wakati huo huo, walikuwa na wasiwasi juu ya utendaji duni wa Biden. Lakini 7kiongozi mwenza wa kampeni ya Trump alipuuzilia mbali gumzo kuhusu iwapo Wanademokrasia watajaribu kuteua mtu mwingine badala ya Biden.
"Kuna wataalam wengi wa kisiasa kwenye X, kwa hivyo tutasikia mengi kutoka kwao, nina hakika, siku chache zijazo kwa sababu wote wameendesha kampeni nyingi," alisema LaCivita kwa kejeli. "Lakini njia pekee hilo linaweza kutokea ni kwa Joe Biden kuachia kwa hiari, na hatafanya hivyo."
Mdahalo wa Alhamisi unaweza kubakia kwenye akili za wapiga kura kwa muda mrefu ujao wakati ambapo Biden na Trump hawajapangiwa kukutana tena kwenye jukwaa kwa siku 75 nyingine.Biden asafisha njia kwa tiketi ya kuwania urais Georgia
LaCavita alisema Trump atakuwa kwenye mdahalo ujao "huku kengele zikiwa zimewashwa." Msemaji wa kampeni ya Biden Kevin Munoz alithibitisha kuwa Biden pia atahudhuria mchuano wa marudiano.
Lakini faraghani, washauri wa Biden walisema kuwa kampeni hiyo haitaweza kushinda au kupotea katika mkutano mmoja, mazungumzo au mdahalo. Walitaja mipango ya kudumisha ratiba kali katika wiki na miezi ijayo.
Siku ya Ijumaa, Biden alipangiwa kufanya kampeni huko North Carolina wakati Harris alikuwa Nevada. Bado lakini, wafuasi wa Biden walipambana kujipa matumaini mara baada ya mdahalo huo.Biden, Trump wazoa ushindi kinyang´anyiro cha ´Jumanne Kuu´
"Huo ulikuwa utendakazi mbaya zaidi katika historia ya midahalo ya urais iliyoonyeshwa kwenye televisheni," Tim Miller, mwanamkakati wa zamani wa chama cha Republican aliyegeuka kuwa mfuasi sugu wa Biden, alisema katika chumba cha waandishi habari baada ya mdahalo huku akitikisa kichwa kwa kutoamini.