BERLIN:Waarabu wanne wafungwa kwa kutaka kushambulia maneneo ya Wayahudi nchini Ujerumani.
26 Oktoba 2005Mahakama moja ya hapa Ujerumani imewatia hatiani Waarabu wanne kwa kula njama za kushambulia maeneo ya Wayahudi katika mji wa Berlin na Duesseldorf.
Watu hao wanne wamehukumiwa vifungo kati ya miaka mitano na minane jela.
Washtakiwa hao wawili raia wa Jordan,Mpalestina mmoja na Mualgeria,walitiwa mbaroni mwaka 2002,baada ya polisi kuendesha msako mkali.
Awali muendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Ujerumani,alisema watu hao wanne walikuwa ama ni wanchama au washabiki wa kikundi cha Al Tawhid,ambacho kina msimamo mkali na pia kinaaminika kina uhusiano na kikundi cha al-Qaeda kinaongozwa na mpiganaji raia wa Jordan,Abu Musab al Zarqawi.
Kesi dhidi ya watu hao kwa sehemu kubwa iliegemea zaidi ushahidi uliotolewa na mtu aliyekamatwa siku moja na watu hao,ambaye alidai aliwahi kuwa mlinzi wa karibu wa Osama bin Laden.