BERLIN:Ujenzi wa kumbukumbu ya Wayahudi kuendelea
14 Novemba 2003Matangazo
Mnara wa Kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi uliopangwa kujengwa nchini Ujerumani utajengwa mjini Berlin kwa kutumia bidhaa za kampuni moja ya kemikali yenye historia na Manazi wa zamani licha ya kupingwa na baadhi ya viongozi wa Kiyahudi. Wadhamini wanaosimamia mradi huo wamesema ujenzi utaendelea juu ya kwamba mnara huo wa kumbukumbu utakuwa na bidhaa zilizotengenezwa na Degussa AG kampuni iliyohusisha na gasi waliyotumia Manazi kuwaangamiza Mayahudi katika kambi za mateso wakati wa Vita Kuu Vikuu vya Pili vya Dunia. Kwa mujibu wa msemaji wa mradi huo uamuzi wa kuendelea kutumia bidhaa za Degussa umetolewa kwa kuzingatia mambo yote mawili kwamba unatekelezeka na uadilifu baada ya majadiliano ya muda mrefu na mazito.