1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wanazi mamboleo waandamana nchini Ujerumani.

21 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEj7

Mamia ya waungaji mkono wa mrengo wa kulia nchini Ujerumani wamefanya maandamano mjini Berlin na Nuremberg, siku tatu baada ya kumbukumbu ya kifo cha makamu wa Adolf Hitler, Rudolf Hess.

Katika mji mkuu wa Ujerumani , kiasi cha waungaji mkono hao wa mrengo wa kulia wapatao 500 waliandamana kutoka katika eneo la wazi la Alexanderplatz hadi katika kitongoji kimoja cha eneo la mashariki.

Mjini Nuremberg, kiasi cha waungaji mkono hao 350 wa chama cha National Democratic Party, walifanya maandamano licha ya juhudi za viongozi wa mji huo kuzuwia mkusanyiko huo.

Wanachama hao wa Wanazi mamboleo walikuwa wanakutana katika miaka ya nyuma katika mji wa kusini wa Wunsiedel, ambako Hess amezikwa, lakini sheria mpya za kupunguza maandamano zimeruhusu mahakama kuzuwia mikusanyiko.

Lakini mahakama nyingine zimeruhusu maandamano hayo ya mji wa Nuremberg kufanyika.