BERLIN : Mkuu wa waajiriwa Volkswagen ataka kujiuzulu
9 Julai 2005Mkurugenzi wa waajiriwa katika kampuni ya magari ya Ujerumani Volkswagen amewasilisha baruwa ya kujiuzulu kwake.
Volkswagen imesema katika taarifa kwamba Peter Hartz amewasilisha pendekezo hilo la kujiuzulu kwa bodi ya usimamizi ya kampuni hiyo lakini haikusema lini bodi hiyo itatowa uamuzi wake . Hatua yake hiyo inakuja huku kukiwa na kashfa ya hongo na rushwa ambayo imekuwa ikifichuliwa dhidi ya kampuni hiyo kubwa kabisa ya kutengeneza magari barani Ulaya kwa wiki kadhaa zilizopita.
Repoti kadhaa za vyombo vya habari zimedokeza kwamba menejimenti ya kampuni hiyo imekuwa ikiwatumia inavyotaka wajumbe wa baraza la kazi la kampuni hiyo kuidhinisha hatua kali za mageuzi za kampuni hiyo.
Hartz amekanusha kuwa na kosa lolote lile.