1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN Mikutano ya manazi wa kileo huenda ipigwe marufuku.

18 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFcf

Bunge la Ujerumani limeanza kujadili mswada wa sheria inayonuiwa kupunguza uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara ya manazi wa kileo. Serikali ya muungano ya kansela, Gerhard Schroeder, inataka mswada huo upitishwe ili kuikomesha mikutano hiyo. Viongozi wa upinzani kwa upande wao wanataka eneo la lango la Brandenburg na Holocaust Memorial lipigwe marufuku kusifanyike mikutano hiyo. Manazi wa kileo wanataka kuandamana kwenye lango hilo la Brandenburg tarehe 8 mwezi Mei, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kushindwa kwa Ujerumani ya manazi. Jaji wa zamani Dieter Grimm ameonya dhidi ya kulipiga marufuku eneo hilo, akisema katiba ya Ujerumani iliyoandikwa baada ya vita inaruhusu raia kufanya mikutano ila tu kwenye maeneo ambayo heshima ya waathiriwa wa mauaji ya halaiki ya wayahudi itaathiriwa.