BERLIN: Mageuzi makuu yafanywe Benki ya Dunia
22 Mei 2007Matangazo
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel,Muhammad Yunus wa Bangladesh,ametoa mwito wa kufanywa mageuzi makuu katika Benki ya Dunia.Amesema,rais wa Benki ya Dunia,Paul Wolfowitz atakapondoka madarakani mwezi ujao,taasisi hiyo iwe “Benki ya Masikini”. Yunus alikuwa akizungumza katika kongamano la Benki ya Dunia kuhusika na uwekezaji barani Afrika.Wakati huo huo waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani,Heidemarie Wieczorek-Zeul alisema,wadhifa wa mkuu wa benki hiyo,ambao kwa kawaida hushikwa na Mmarekani,katika siku zijazo, nchi zinazoendelea zingepewa nafasi ya kushiriki.