BERLIN: Kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi
10 Mei 2005Matangazo
Kumbukumbu ya maangamizi,iliyozusha mabishano itafunguliwa rasmi hii leo mjini Berlin.Ujenzi wa Kumbukumbu hiyo ya Wayahudi waliouawa barani Ulaya ni uwanja wenye matofali ya rangi ya majivu na ni karibu ya Lango la Brandenburg.Ujenzi wa matofali hayo 2,700 ya zege ulichukua miaka miwili.Sherehe hiyo itahudhuriwa na kiasi ya wageni 1,000 ikiwa ni pamoja na rais wa Ujerumani Horst Köhler,Kansela Gerhard Schroeder na watu walionusurika na maangamizi hayo makuu.