1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela apata tuzo ya Wayahudi.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79L

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa tuzo ya mwaka huu ya Leo Beck. Baraza kuu la wayahudi nchini Ujerumani limesema kuwa limemteua Merkel kwa ajili ya tuzo ya mwaka huu kwa juhudi zake za kuimarisha maelewano baina ya Wayahudi na wasio Wayahudi pamoja na uhusiano baina ya Ujerumani na Israel. Katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo katika sherehe hizo mjini Berlin, kansela amesema Ujerumani ina wajibu wa kihistoria kusaidia kulinda usalama wa taifa la Kiyahudi.

Amesema , ni pamoja na kuwapo tayari kuunga mkono vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran iwapo itashindwa kukubaliana na madai ya jumuiya ya kimataifa kuhusiana na mpango wake wa kinuklia.