Berlin. Aliyejaribu kumuua Hitler akumbukwa.
16 Novemba 2007Matangazo
Katika sherehe maalum mjini Berlin, waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung ameadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Claus Schenk von Stauffenberg, afisa wa jeshi la Ujerumani , ambaye alijaribu kumuua kiongozi wa wanazi Adolf Hittler wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Jung amekitaja kitendo cha jaribio la kumuua Hitler , tukio la ukombozi, na kusema kuwa von Stauffenberg alikuwa mfano kwa majeshi ya Ujerumani. Mwanahistoria wa Ujerumani , hata hivyo, ameonya dhidi ya kumfanya von Stauffenberg kuwa shujaa wakati alikuwa akiunga mkono malengo ya utawala wa Wanazi kwa miaka kadha kabla ya kugeuka.