Miito yatolewa juu ya mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa
22 Juni 2023Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ameuambia mkutano huo wa kilele kwamba jumuiya ya kimataifa lazima iangalie uwezekano wa kuanzisha tozo ya hewa ukaa duniani ili kuharakisha malengo ya kupunguza uzalishaji wa hewa hiyo chafu ya kaboni. Amesema tozo hiyo ilikuwepo katika nchi za Umoja wa Ulaya na yamepatikana mabilioni ya euro.
Von der Lyen amesema kulikuwepo mapato kutoka kwenye tozo ya hewa chafu ya kaboni. Zilipatikana takriban euro bilioni 142 na wakati huo huo uzalishaji wa hewa ya kaboni ulipungua kwa asilimia 35.
Von der Leyen ameserma anapendekeza mpango huo wa kuwatoza wote wanaozalisha hewa chafu ya kaboni duniani. Amesema tozo ya hewa ya kaboni ni mojawapo ya njia bora za kupunguza uzalishaji hewa ya ukaa ambapo wachafuzi wa mazingira watabidi wafikirie mara mbili iwapo watataka kuendelea kulipa fedha nyingi kwa uchafuzi wa mazingira au watabidi wabadilike na kuelekea katika matumizi ya yanayozingatia ulinzi wa mazingira.
Soma:Benki ya Dunia yazindua mkakati kusaidia nchi zenye majanga
Kwa upande wake mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Kristalina Georgieva amesema nchi tajiri zimefikia malengo ya kutenga dola bilioni 100 kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na umasikini katika nchi zinazoendelea. Georgieva amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wa kilele wa kufadhili nchi zinazokabiliwa na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa huko mjini Paris.
Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso amesema nchi yake inapanga kuandaa mkutano wa kilele wa nchi zilizo na mito kwenye misitu kuliangaliam uaidi swala la mabadilikoya hali ya hewa.
Wakati huo huo katika maswala yanayohusu kuzipunguzia nchi mzigo wa madeni waziri wa uchumi wa Ufaransa amesema viongozi katika mkutano wa kilele wa fedha duniani wanakaribia kutia kusaini mikataba ya kurekebisha madeni ya Zambia na Sri Lanka kwa makubaliano na mkopeshaji mkuu wa nchi zote mbili ambaye ni China.
Soma:
Zambia, mzalishaji mkuu wa madini ya shaba barani Afrika, imeshindwa kulipa deni lake la nje la dola bilioni 18.6 mnamo mwaka 2020 na Sri Lanka ikafuatia mwaka jana wa 2022, kwa kukosa pia kulipa mkopo wa dola bilioni 46.
Ufaransa imesema China imo kwenye bodi ya kujadili marekebisho ya madeni ya nchi zote mbili katika mkutano wa kilele wa mjini Paris unaohudhuriwa na Waziri Mkuu wa China Li Qiang miongoni mwa viongozi wengine wa dunia.
Naye waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif amekutana na mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF pembezoni mwa mkutano huo wa kimataifa akitarajia nchi yake itafunguliwa kiasi cha dola bilioni 6 za kuisaidia na wakati huo huo itapewa mkopo kwa awamu mbili wa dola bilioni 1.1 ambao ulisitishwa tangu mwezi Novemba.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito wa kuendeleza mapambano dhidi ya majanga ya umasikini na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwanaharakati wa mazignira wa Uganda, Vanessa Nakate amezitaka nchi tajiri zifute madeni kwa nchi masikini na badala yake wazipecnhi hizo fedha za kukabiliana na majanga yanayosababishwa na mbadiliko ya hali ya hewa. Nakate amesema nchi tajiri mara zote zinaahidi maendeleo kwa jamii maskini lakini nishati inayopataikana inakwenda kwingine na faida inaingia kwenye mifuko ya watu ambao tayari ni matajiri wa kupindukia.
Benki ya Dunia imesema imezindua mpango wa kusitisha kwa muda ulipaji wa madeni kwa nchi zilizokumbwa na maafa na shirika la fedha la kimataifa IMF limesema limefikia lengo lake la dola bilioni100 kwa ajili ya nchi zilizo hatarini kutokana na uharibifu wa hali ya hewa.
Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF zimelaumiwa kwa kutochangia kwenye malengo ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa katika maamuzi ya utoaji wa mikopo na kwamba taasisi hizo zimetawaliwa na nchi tajiri kama Marekani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mfumo wa fedha wa kimataifa uko katika hali mbaya.
Vyanzo: AFP/AP