1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Dunia yaingiwa wasiwasi na mikakati ya Tanzania

Daniel Gakuba
3 Oktoba 2018

Benki ya Dunia imesema sheria mpya ya Tanzania, inayotoa adhabu kwa mtu yeyote atakayekosoa takwimu zinazotolewa na serikali itakwamisha kutolewa takwimu za kuaminika.

https://p.dw.com/p/35vhm
USA Weltbank Sitz in Washington
Picha: picture-alliance/epa/S. Zaklin

Benki ya Dunia imesema imetiwa wasiwasi na sheria mpya ya Tanzania, ambayo inatoa adhabu kwa mtu yeyote atakayekosoa takwimu zinazotolewa na serikali. Benki hiyo imesema sheria ya namna hiyo itakwamisha kutolewa kwa takwimu zinazoaminika.

Mwezi uliopita, bunge la Tanzania liliidhinisha sheria ambayo inaweka vikwazo na kifungo cha miaka isiyopungua mitatu jela, kwa mtu yeyote atakayetilia shaka uhalisia wa takwimu zinazotolewa na vyombo rasmi.

Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo alisema sheria hiyo ilihitajika ili kuweza kuheshimisha viwango. Benki ya Dunia imesema sheria hiyo ambayo haijatiwa sahihi na Rais John Magufuli, haiendani na viwango vya kimataifa.

Wapinzani na wakosoaji wengine wamesema sheria hiyo imewekwa mahsusi kuendeleza ukandamizaji dhidi ya wanaokosoa ufanisi wa serikali kisiasa na kiuchumi.