Benki ya Dunia yaidhinisha kitita cha ufadhili kwa Ethiopia
31 Julai 2024Matangazo
Katika taarifa, benki hiyo imesema kuwa itatoa ruzuku ya dola bilioni 1 na dola milioni 500 nyingine kwa riba nafuu, hii ikiwa sehemu ya msaada wa kwanza wa bajeti uliotolewa kwa Ethiopia.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa benki hiyo inapanga kutoa takriban dola bilioni 6 kwa mipangilio mipya katika muda wa miaka mitatu ijayo ya fedha na kusaidia mageuzi ya kiuchumi kupitia msaada wa bajeti unaotolewa haraka.
Kulingana na maafisa wa Ethiopia, pesa hizo ni sehemu ya ufadhili wa dola bilioni 10.7 wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia na wafadhili wengine.