1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yaruhusu bendera za jamii asilia kupepea kombe la dunia

7 Julai 2023

Bendera za watu wa jamii asilia za Australia na New Zealand kwa mara ya kwanza zitapeperushwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Wanawake yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 20 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4Tb6l
Australien Frauenfussball Philippines vs Papua New Guinea
Timu ya taifa ya Australia ambaye itakuwa mwenyeji wa mashindano yaa kombe la dunia mwakan huu.Picha: Luis Veniegra/ZUMAPRESS/IMAGO IMAGES

 
Bendera za watu wa jamii asilia za Australia na New Zealand kwa mara ya kwanza zitapeperushwa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Wanawake yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 20 mwaka huu katika viwanja mbalimbali katika mataifa ya Australia na New Zealand.

Hii ni baada ya mamlaka inayoongoza soka ulimwenguni kufikia makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kanuni za siku za mechi za FIFA kwenye viwanja vya mashindano.

Soma zaidi :Kifaa cha mionzi kilichopotea Australia chapatikana

Bendera zote tatu za jamii ya Austalia zitaonyeshwa katika kipindi chote cha mashindano, bendera za jamii ya watu wa asili ya Waboriginal, Torres Strait Islander za Australia na ile ya Maori maarufu kwa jina la Tino Rangatiratanga ya nchini New Zealand na bendera za mataifa mengine yanayoshiriki mashindano hayo pia zitakuwa zinapepea wakati wa mshindano hayo.

Tangu kutawaliwa kwa Australia na walowezi wa Kizungu, Waaustralia wa asili ya Aboriginal na Torres Strait Islander wamepitia nyakati ngumu ikiwemo kutothaminika na kuheshimiwa kwa utamaduni wao na madhila chungunzima pamoja na kunyimwa haki za uraia.

Soma zaidi:Scholz aunga mkono Ujerumani kuwa mwenyeji wa soka la wanawake 

Schweiz Genf | FIFA Präsident Gianni Infantino
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino.Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Rais wa FIFA Gianni Infantino amethibitisha uamuzi huo hii leo wakati wa wiki ambayo inaadhimisha watu wa jamii za kiasili nchini Australia.

Rais huyo wa FIFA amenukuliwa akisema kuwa "FIFA imekubali ombi lililotolewa na Ushauri wake wa 
Jopo la utamaduni pamoja na shirikisho la Kandanda nchini Australia na New Zealand. Uamuzi huo uliungwa mkono na serikali za Australia na Aotearoa New Zealand".

Infantino ameongeza kuwa "Bendera hizi muhimu zinaonyesha roho ya kuheshimiana, utambulisho wa kitaifa, na utambuzi wa tamaduni za kiasili kwa wenyeji wetu."

Uamuzi huo umeungwa mkono na Afisa mkuu mtendaji wa shirikisho la Soka nchini New Zealand Andrew Pragnell huku akionyesha bendera ya Tino Rangatiratanga inayoonyesha ishara yenye nguvu kwa jamii ya watu wa New Zealand.

Pragnell anasema ''Kombe la Dunia la 2023 linatoa fursa ya kuunda njia ya mashindano yanayobadilika na uingiliana na waandaji wake katika matoleo yajayo na hasa katika kutambua haki za wenyeji duniani kote."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kandanda Australia James Johnson amasema uamuzi huo umeunga mkono idhini yao inayoendana na maadili ya shirikisho la soka nchini humo kwa kuonyesha utofauti wa mashindano na ushirikishwaji katika msingi na maono kwa mashindano hayo makubwa duniani.

Fussball I Africa Cup I Frauen I Marokko
Morocco ni moja ya timu kutoka Afrika ambayo itashiriki michuano yabkombe la dunia kwa wanawake huko Australia na New Zealand kuanzia Julai 20 mwaka huu.Picha: Gavin Barker/Sports Inc/empics/picture alliance

Kombe la Dunia la Wanawake litaanza Julai 20 kwa New Zealand kucheza dhidi ya Norway huko Auckland na Australia dhidi ya Ireland mjini Sydney. 

Timu nne kutoka Afrika zinashiriki mashindano hayo nazo ni Zambia, Nigeria, Afrika Kusini na Morocco.