Bayern waduwazwa na Bochum 3-2
19 Februari 2024Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel amekiri kwamba kushinda taji la Bundesliga msimu huu "ni kama ndoto" baada ya kupoteza dhidi ya Bochum jana Jumapili na kuiacha Bayer Leverkusen pointi nane kileleni.
Kazi ya Thomas Tuchel kama kocha wa Bayern Munich bado iko salama kwa sasa licha ya kupoteza mechi tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Mei 2015.
Soma pia: Thomas Tuchel abeba lawama kufuatia kipigo cha 3-0
Alipoulizwa ikiwa kibarua chake kipo hatarini, Tuchel alisema "hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo". Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen aliwaambia wanahabari Tuchel "bila shaka" kocha huyo atakuwa dimbani dhidi ya Leipzig siku ya Jumamosi.
Bayern walipoteza mechi ya jana licha ya kutangulia kupata bao dakika ya 14 kupitia mchezaji Jamal Musiala, lakini Bochum waliongeza juhudi na kujibu mara mbili kupitia Takuma Asano na Kevin Schollterbeck kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Kipindi cha pili kunako dakika ya 77 beki wa Bayern Dayot Upamecano alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Bochum walitumia fursa na kugongelea msumari wa tatu kupitia mchezaji Kevin Stöger.
Bao la dakika za jioni la Harry Kane limeongeza idadi yake ya mabao msimu huu lakini bado waliangukia pua.
Alipoulizwa ikiwa kibarua chake kipo hatarini, Tuchel alisema "hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo".
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen aliwaambia wanahabari Tuchel "bila shaka" kocha huyo atakuwa dimbani dhidi ya Leipzig siku ya Jumamosi.
Kutangulia sio kufika
Bayern walipoteza mechi licha ya kutangulia kupata bao dakika ya 14 kupitia mchezaji Jamal Musiala, lakini Bochum waliongeza juhudi na kujibu mara mbili kupitia Takuma Asano na Kevin Schollterbeck kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Kipindi cha pili kunako dakika ya 77 beki wa Bayern Dayot Upamecano alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Bochum walitumia fursa na kugongelea msumari wa tatu kupitia mchezaji Kevin Stöger. Bao la dakika za jioni la Harry Kane limeongeza idadi yake ya mabao msimu huu lakini bado waliangukia pua.
Kichapo cha hivi punde kimewaacha mabingwa hao mara 11 pointi nane nyuma ya vinara Leverkusen. Tuchel alisema kikosi chake kitaendelea kupambana ili kupunguza pengo hilo zikiwa zimesalia mechi 12.
"Tulipoteza mechi tatu, jambo ambalo bila shaka ni chini ya matarajio yetu wenyewe. Tena, hii ya leo haiendani na mechi mbili zilizopita. Lakini tuna adhabu na kadi nyekundu ambayo hufanya maisha kuwa tofauti sana. Leo ni kwamba tulikuwa na nafasi nyingi na hatukubadilisha makosa. Kwa hivyo leo tumeadhibiwa. " alisema Tuchel.
Historia imejirudia
Ikumbukwe kwamba Mnamo Mei 2015, Bayern ilipoteza kwa Leverkusen, kisha dhidi ya Barcelona kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya Augsburg kushinda 1-0 mjini Munich kwenye mechi Bundesliga. Lakini Bayern walikuwa tayari wamehakikishiwa ubingwa wa Bundesliga msimu wa pili chini ya kocha Pep Guardiola.
Katika mechi nyengine Borussia Dortmund na VfL Wolfsburg waligawana pointi katika sare ya 1-1 siku ya Jumamosi, na kuwaacha Dortmund katika nafasi ya nne kwenye jedwali la Bundesliga, pointi tano nyuma ya Stuttgart walio katika nafasi ya tatu.
Mchezo huo ulikatizwa mara kwa mara wakati watazamaji waliporusha mipira ya tenisi uwanjani katika maandamano yanayoendelea ya mashabiki kupinga uwekezaji wa kigeni uliopangwa katika Bundesliga.
Soma pia:Leverkusen haishikiki katika Bundesliga
Vinara wa Bundesliga Bayer Leverkusen waliendeleza msururu wao wa kutoshindwa katika mashindano yote msimu huu hadi kufikia rekodi ya mechi 32, baada ya ushindi wa 2-1 huko Heidenheim.
Kocha Xavi Alonso mumeshaanza kujianda kushinda taji la Bundesliga?
"Kusema kweli hatufikirii, tunafikiria kujiandaa kwa kila mchezo, hiyo ndiyo mbinu bora kufikia sasa, tumekuwa tukifanya vizuri na haitabadilika, ili tuone jinsi gani tunaweza kufika mbali. Lakini tuko katika njia nzuri na tutaona." Alijibu Alonso.
Leipzig iliwashinda Gladbach 2-0 na kufufua matumaini yao ya kutinga hatua ya nne bora baada ya wachezaji Xavi Simons na Loïs Openda kucheka na wavu dakika ya 14 na 57 mtawalia.
Katika msimamo wa jedwali la Bundesliga Darmstadt wapo mkiani wakiwa na pointi 12 baada ya mechi 22, Mainz imetulia katika nafasi ya 17 kwa pointi 15 huku FC Köln ikiiwa juu yake pointi moja mbele.
Je Hatma ya Alonso Leverkusen ikoje?
Huku haya yakijiti Liverpool wanamtaka kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso na mkurugenzi wao wa michezo Simon Rolfes kwa msimu mpya, kulingana na jarida la Football Insider .
Jarida hilo limenukuu "vyanzo vya karibu", likisema wawili hao walikuwa juu ya orodha fupi ya viongozi wa Premier League kuchukua nafasi ya meneja Jürgen Klopp, ambaye ataondoka baada ya msimu huu, pamoja na Jörg Schmadtke, aliyeondoka Anfield mwishoni mwa Januari.
Alonso aliichezea Liverpool kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 na kushinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2005. Pia alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid, pamoja na Kombe la Dunia la 2010, na Euro 2008 na 2012 akichezea timu ya taifa ya Uhispania.
Rolfes mchezaji wa zamani wa Ujerumani na Leverkusen amekuwa mkurugenzi wa michezo tangu 2022 na amekuwa muhimu katika kuweka pamoja kikosi cha sasa cha Leverkusen chenye mafanikio.
Miongoni mwa wanaohusishwa na kuchukua mikoba ya Klopp ni pamoja na kocha wa zamani wa Bayern Julian Nagelsmann, meneja wa Brighton Roberto de Zerbi na Ruben Amorim wa Sporting Lisbon.