Barrett aapishwa jaji wa Mahakama ya Juu Marekani
27 Oktoba 2020Chaguo la Trump kujaza nafasi iliyoachwa kufuatia kifo cha aliyekuwa jaji wa kiliberali marehemu Ruth Bader Ginsburg kimsingi linafungua enzi mpya ya maamuzi kuhusu utoaji mimba, ulinzi wa huduma za afya na hata kuchaguliwa kwa Trump mwenyewe. Wademocrat walishindwa kuzuia matekeo hayo, ambayo ni jaji wa tatu kuchaguliwa na Trump kwenye mahakama hiyo, wakati Warepublican wakiendelea na harakati za kuifanyia mageuzi idara ya mahakama.
Soma pia: Donald Trump kumtaja Barrett mrithi wa Ginsburg
Bibi Barret mwenye umri wa miaka 48 ameanza kazi rasmi, ikiwa ni uteuzi wake wa maisha wa kuwa jaji wa 115 na kuimarisha nguvu za mahakama ya juu kuegemea mkondo wa mrengo wa kulia. Akizungumza wakati wa hafla ya kumuapisha jaji huyo katika Ikulu ya White House, Trump alisema hii ni siku ya kihistoria kwa Marekani "Leo Jaji Barrett anakuwa sio tu mwanamke wa tano kuhudumu kwenye mahakama ya juu kabisa ya nchi yetu lakini pia mama wa kwanza wa watoto wanaokwenda shule kuwa jaji wa mahakama ya juu - muhimu sana."
Barrett alapa kufanya kazi yake bila hofu wala upendeleo. "Ahsante pie kwa Seneti kwa kutoa idhini yake kwa uteuzi wangu. Nnashukuru kwa imani mliyonionyesha na naahidi kwenu na kwa Watu wa Marekani kuwa nitatekeleza majukumu yangu kwa uwezo wangu wote."
Kura hiyo ya Seneti ni ya kwanza kufanywa karibu mno na uchaguzi wa rais, na ya kwanza katika nyakati za sasa kufanywa bila uungwaji mkono kutoka kwa chama cha wajumeb wachache. Barrett alipigiwa kura 52 dhidi ya 48.
Soma pia: Trump kumteuwa mwanamke katika Mahakama ya Juu
Barrett, jaji wa mahakama ya rufaa kutoka jimbo la Indiana, anatarajiwa kula kiapo cha mahakama leo kitakachoongozwa na Jaji Mkuu John Roberts katika sherehe ya faragha ili kuanza kushiriki katika shughuli za mahakama hiyo.
Wademocrat walihoji kwa wiki kadhaa kuwa kura hiyo inaharakishwa vibaya na kusisitiza kuwa inapaswa kuwa jukumu la mshindi wa uchaguzi wa Novemba 3 kumteuwa jaji mpya.
Trump alisema anataka kumtangaza haraka jaji wa tisa kwenye jopo la mahakama ya juu ili kutatua migogoro ya uchaguzi na anatumai kuwa majaji hao wataifuta sheria ya afya inayofahamika kama Obamacare.
Ni Seneta mmoja pekee wa Republican, Susan Collins aliyepiga kura kupinga uteuzi huo akisema sio haki kwa seneti kupiga kura ya aina hiyo kabla ya uchaguzi
AP