Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuijadili Sudan
26 Oktoba 2021Matangazo
Wanadiplomasia wanasema suala hilo limetokana na ombi la mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ireland, Norway na Estonia.
Wajumbe wa Baraza hilo ambao wanahitimisha ziara yao nchini Mali na Niger watarejea mjini New York mchana wa leo, kwa hivyo mkutano huo umepangwa kufanyika alasiri.
Jeshi la Sudan lilijinyakulia madaraka jana Jumatatu, likamkamata waziri mkuu na maafisa wengine wa serikali ya mpito, jambo ambalo limezusha maandamano katika maeneo tofauti ya taifa hilo kwa wakati huu, yenye kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.
Mapinduzi hayo ya kijeshi yanatishia kuhujumu kwa hatua zilizopigwa na taifa hilo kuelekea demokrasia.