Baraza la mawaziri Ujerumani laidhinisha bajeti ya 2025
17 Julai 2024Matangazo
Bajeti hiyo imekuwa mada kuu ya majadiliano kwa wiki kadhaa ndani serikali ya muungano ya Kansela Olaf Scholz.
Bajeti hiyo ya euro bilioni 480.6, imepungua takriban bilioni 8 ikilinganishwa na mwaka huu.
Viongozi wa serikali ya Ujerumani hatimaye waafikiana kuhusu bajeti
Pendekezo la awali, ambalo lilikubaliwa na viongozi wa serikali ya muungano mapema mwezi huu, lilipingwa vikali na wakosoaji kwa madai kwamba halikuzingatia vya kutosha kuimarisha jeshi na kuchochea ukuaji.
Waziri wa Fedha Christian Lindner amepongeza makubaliano hayo na kuyataja kama "mwanzo wa mabadiliko ya kiuchumi" kwa Ujerumani.
Bajeti hiyo sasa ni lazima ipitishwe na wabunge, katika kura ambayo huenda ikafanyika mnamo Novemba.