Barabara muhimu zafunguliwa Kivu Kaskazini
2 Machi 2023Maeneo hayo ni pamoja na Masisi, Rutshuru na maeneo mengine yanayodhibitiwa na kundi la wapiganaji wa M23.
Kufunguliwa tena kwa barabara hizo na vijiji vinavyo sambaza vyakula katika jiji hili, kumetangazwa wakati huu ambapo mamia ya malori yakubeba mizigo, yalianza kuwasili mjini jana jioni baada ya majuma kadhaa yakiwa yamezuiliwa na waasi wa M23 katika vijiji mbalimbali vinavyo shuhudia machafuko kwa zaidi ya mwezi moja sasa.
Hata hivyo, akiuhutubia mkutano wa wanahabari ,luteni kanali Guillaume Njike msemaji wake gavana wakijeshi ,amedai kuwa hii ni njia pekee ya kuwasaidia maelfu wa raia wanaohangaishwa na vita.
Raia wana hofu kuhusiana na ukosefu wa chakula
Wakati hatua hii ya mamlaka yakijeshi imepongezwa na maafisa wa idara za usafiri jimboni humu, maafisa wa asasi za kiraia wameonekana kuwa na mashaka kufuatia mapigano na ukosefu wa usalama kwenye maeneo yalio tajwa katika tangazo hilo .
Awali, raia wanao ishi katika vijiji wilayani Rutshuru baadhi ikiwa ni wale wanao tegemea kilimo,walidai kuingiwa na hofu kufuatia ukosefu wa chakula unaotokana nakuzuiliwa kwao kutoelekea mashambani na kundi hilo la wapiganaji.
Hata hivyo wakaazi wa mji huu wa Goma waliotengwa na mitaa inayozalisha chakula kwa sababu ya vita,wamekuwa pia na hisia tofauti .
Msururu wa magari yenye mizigo kutoka maeneo yanayoshikiliwa na waasi yameendelea kuingia mjini Goma nakushangiliwa na maelfu wa raia.