1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Bangladesh yakabiliwa na maandamano zaidi

2 Agosti 2024

Bangladesh imekabiliwa na maandamano zaidi dhidi ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina na serikali yake, waandamanaji wakitaka haki kwa zaidi ya watu 200 waliouwawa katika maandamano ya mwezi uliopita yaliyokuwa na machafuko.

https://p.dw.com/p/4j35a
Bangladesh Waandamana Dhaka
Ndugu na jamaa za wanafunzi waliowekwa vizuizini wakiwa katika maandamano ya kupingwa kukamatwa kwa wapendwa wao.Picha: DW

Haya yanafanyika licha ya tangazo la mageuzi katika mfumo wa utoaji kazi, ambao ndio uliosababisha wiki za maandamano. Zaidi ya waandamanaji 2,000 wamekusanyika katika mji mkuu Dhaka, baadhi wakitoa kauli za kumtaka Hasina aondoke madarakani na wengine wakiimba nyimbo za kudai haki kwa wahanga. Polisi wamekabiliana na waandamanaji katika eneo la Uttara huko Dhaka huku baadhi ya maafisa hao wakifyatua mabomu ya kutoa machozi na maguruneti ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe. Haya ndiyo maandamano ya wanafunzi ya hivi karibuni dhidi ya serikali ya waziri mkuu huyo, maandamano ambayo hayaonyeshi dalili za kufifia.