1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bandari ya msumbiji yaripoti kushuka kwa kibiashara

21 Januari 2025

Bandari kubwa zaidi nchini Msumbiji katika mji mkuu Maputo, imeripoti kushuka kwa moja asilimia ya shughuli za kibiashara kwa mwaka 2024 kutokana hasa na maandamano ya baada ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4pRBI
Kenia Verlade-Hafen in Mombasa
Picha: Photoshot/picture alliance

Maandamano hayo yalilazimisha mpaka na barabara kadhaa kufungwa nchini humo.

Waendeshaji wa bandari hiyo wamesema kwamba shughuli za kibiashara za usafirishaji mizigo kwenye bandari hiyo mnamo mwaka 2024 zilishuka na kufikia tani milioni 30.9 ikilinganishwa na tani milioni 31.2 zilizorekodiwa kusafirishwa mwaka 2023.

Taarifa ya kampuni inayohusika na maendeleo katika bandari ya Maputo, kushuka huko kwa shughuli za kibiashara kumesababishwa na hatua mbali mbali na hasa kufungwa kwa mpaka na barabara kwa siku chungunzima kutokana na maandamano yaliyosababishwa na vurugu za kisiasa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW