1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUmoja wa Falme za Kiarabu

Balozi wa serikali ya Afghanistan ajitambulisha UAE

23 Agosti 2024

Mwakilishi wa Afghanistan amekabidhi hati za utambulisho wa kibalozi katika Umoja wa Falme za Kiarabu akiwa wa pili baada ya China kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/4jrV8
Makubaliano kati ya UAE na Taliban
Taliban na Umoja wa Falme za Kiarabu wamekuwa wakiashiria kuimarisha uhusiano kwa muda sas. Pichani wawakilishi wa pande hizo mbili wakibadilishana nyaraka katika hafla ya kutiliana saini, Mei 24, 2024Picha: Ali Khara/REUTERS

Nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta imesema imejizatiti kujenga mahusiano ili kuwasaidia watu wa Afghanistan.

Kustawi kwa mahusiano ya Umoja wa Falme za Kiarabu na serikali ya Taliban kunajumuisha kusimamiwa bandari za Afghanistan na kampuni ya Falme za Kiarabu baada ya majeshi ya Marekani kuondoka nchini Afghanistan na kurejea kwa Taliban katika madaraka.

Hatua ya balozi huyo, Mawlawi Badruddin, ya kukabidhi hati za utambulisho wa kibalozi ni ushindi kwa serikali ya Taliban ambayo haitambuliwi na Umoja wa Mataifa kwa madai ya kuwanyima wasichana haki ya kupata elimu ya shule ya sekondari.