Baerbock: Tunatumai Israel itazuia madhila kwa Wapalestina
11 Desemba 2023Matangazo
Tamko la waziri huyo linaonesha kubadilika kwa kiasi kwa msimamo wa serikali ya Ujerumani ambayo ilikuwa imejielekeza zaidi katika kuiunga mkono Israel ambayo ni mshirika wake.
Katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dubai pembezoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira, Baerbock amesema Ujerumani inatarajia kuiona Israel ikiruhusu misaada zaidi ya kibinadamu ikiingia na hasa Gaza,na kuhakikisha hatua zake za kijeshi zinaelekezwa zaidi kwa walenga na kuepuka kusababisha mauaji ya raia.
Ujerumani imekuwa ikitetea vikali haki ya Israel kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Hamas ya Octoba 7,japo imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji ikiwemo na wayahudi wanaoishi Ujerumani, kutokana na mgogoro wa kibinadamu uliosababishwa Gaza.