Uhuru wa vyombo vya habariUjerumani
Baerbock atahadharisha juu ya matumizi ya akili ya kubuni AI
18 Juni 2024Matangazo
Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari linaloandaliwa na Deutsche Welle (GMF) linaingia siku yake ya pili na ya mwisho hii leo.
Akihutubia kongamano hilo, Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametahadharisha juu ya matumizi mabaya ya akili ya kubuni AI na jinsi teknolojia hiyo inavyoweza kutumiwa kuleta migawanyiko na kuongeza viwango vya ukosefu wa usawa.
Soma pia: Waziri wa Ujerumani Baerbock ziarani Ukraine
Kongamano hilo limekutanisha waandishi na wadau wa habari takriban 1,500 kutoka zaidi ya mataifa 100 ulimwenguni kote ili kujadiliana kuhusu njia za kujenga misingi imara ya uandishi katika nyakati ngumu.