1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock asema Urusi imetengwa kutokana na vita vya Ukraine

22 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amesema Urusi ilikosolewa katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa na katika Baraza la Usalama la umoja huo, na kutengwa kimataifa kufuatia vita vyake nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Wge4
USA | UN-Vollversammlung Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa MataifaPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amesema Urusi ilikosolewa katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa na katika Baraza la Usalama la umoja huo, na kutengwa kimataifa kufuatia vita vyake nchini Ukraine na ukiukaji wake unaoendelea wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Baerbock, aliliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, kwamba Urusi ilikumbwa na ukosoaji mkali ilipojaribu kuhoji juu ya maazimio muhimu ya maendeleo endelevu na afya kimataifa.

Ujerumani kutoa msaada zaidi kwa Ukraine wakati ikiendelöeza harakati za jkuyakomboa maeneo yake yanayokaliwa na Urusi

Ujerumani kutoa msaada zaidi kwa Ukraine wakati ikiendelöeza harakati za jkuyakomboa maeneo yake yanayokaliwa na Urusi

Alisema hayo mjini New York kabla ya kurejea nchini mwake, baada ya kuhudhuria Hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa.

Wakati akiwa New York, Baebock pia alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuufanya Umoja wa Mataifa uwe na uwezo katika siku zijazo pamoja na mageuzi makubwa. Ameongeza kuwa umoja huo unahitaji kuboreshwa.