Baerbock anaonya kutanuka kwa mashambulizi ya Urusi Ulaya
21 Julai 2024Akizungumza na magazeti ya kampuni kubwa ya Funke Media Group, Baerbock amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa "mara kwa mara akipanua shehena yake ya silaha ambayo inatishia uhuru wa Ulaya."
Soma pia: Waziri wa Ujerumani Baerbock ziarani Ukraine
Haya yanajiri huku kukiwa na mjadala ndani ya muungano wa vyama vitatu vinavyotawala nchini Ujerumanijuu ya mipango ya kupokea silaha za nyuklia kutoka Marekani.
Hata hivyo Rolf Mützenich, kiongozi wa wabunge wa chama cha Kansela Olaf Scholz, cha Social Democratic (SPD), ameonya juu athari za silaha hizo, na kuongeza kwamba zinaweza kuzusha mzozo mpana zaidi wa kijeshi barani Ulaya.
Mützenich anakubaliana na hoja ya kuimarishwa kwa uwezo wa ulinzi, lakini amesema Jumuiya ya kujihami ya NATO tayari inavyo vifaa vya kuzuia mashambulizi. Aidha kiongozi huyo amehoji juu ya sababu za makombora hayo kuwekwa ndani Ujerumani pekee.