1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock afuta ziara ya Djibouti

25 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameifuta Djibouti kwenye ratiba ya ziara yake ya mashariki mwa Afrika baada ya ndege yake kushindwa kupewa ruhusa ya kuruka katika anga ya Eritrea.

https://p.dw.com/p/4begk
Annalena Baerbock - Ujerumani - Djibouti
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock, akiwasili Jeddah siku ya Jumatano (Januari 24) baada ya ndege yake kukataliwa kutumia anga la Eritrea ikiwa safarini kuelekea Djibouti.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Badala yake, ndege hiyo ya serikali ya Ujerumani iliyombeba Baerbock ilibadilishiwa mkondo na kutua Jeddah magharibi mwa Saudi Arabia, ambako ujumbe wake ulilala nchini humo.

Waziri huyo alitumai kuendelea na safari yake kwenda Djibouti leo, lakini mwishowe akaifuta, kwa mujibu wa vyanzo vilivyo kwenye ujumbe wake.

Soma zaidi: Ujerumani yashinikiza amani Sudan

Baerbock sasa anaelekea Kenya kama sehemu ya ratiba yake.

Akizungumza baada ya kutua Jeddah, Baerbock alisema kuwa katika eneo lenye mizozo, sio kila kitu kinaweza kufanyika kama ilivyopangwa.

Waziri huyo awali alipanga kufanya mazungumzo nchini Djibouti, Kenya na Sudan Kusini ifikapo Ijumaa.