Bachelet atoa ahadi ya kutoa ripoti ya Uighur
26 Agosti 2022Ripoti hiyo inayosubiriwa kwa muda mrefu kuhusu China ilivyoitendea jamii ya wachache ya Uighur huko jimboni Xinjiang.
Ripoti hiyo inamfanya Bachalet kuwa katika shinikizo kubwa kutoka katika pande zote. Lakini pia kukosekana kwa msimamo madhubuti kwa rais huyo wa zamani wa Chile, katika mkutano wake wa mwisho kwa waandishi wa habari kumezusha ukosolewaji kutoka kwa makundi ya asasi za kiraia, ambayo yamemtuhumu kuchukua mkondo mwepesi dhidi ya China, tangu ile ziara yake ya Mei.
Ripoti kuhusu Xinjiang imekuwa ikifanyiwa kazi kwa miaka mitatu
Ripoti kuhusu Xinjiang imekuwa ikifanyiwa kazi kwa miaka mitatu na kumetolewa ahadi kwa miezi kadhaa lakini imeshindwa kuwekwa hadharani kwa sabababu zisizoeleweka. Zaid Bachalet anasema "Tunaifanyia kazi ripoti hiyo, nimekusudia itolewe kabla ya mwisho wa majukumu yangu kikazi, na tutajaribu. Kwa sasa tumepokea maoni muhimu kutoka kwa serikali ambayo tutahitaji kuyapitia kwa uangalifu kama tunavyofanya wakati wowote. Na kwa taifa lolote."
Kiongozi huyo alitaja mwisho wa mamlaka yake akimaanisha Agosti 31 mwaka huu.
Shinikizo la makundi ya kiraia kwa Bachalet
Makundi ya haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali ya China kwa mateso dhidi ya jamii ya Waislamu wacheche ya Uighur, ambayo inakadiriwa kuwa takribani milioni 10 katika jimbo la mashariki la taifa hilo la Xinjiang, ikiwa pamoja na kufanyishwa kazi za shuruti katika makambi maalumu. Lakini Marekani inaituhumu China kwa mauaji ya wengi, tuhuma ambazo kwa mara kadhaa China imekuwa ikizikanusha.
Mkurugenzi wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la China, Sophie Richardson, amesema namna Bachelet anavyoshughulikia hali ilivyo China sio kwa kiwango cha kuridhisha ukilinganisha na uzito wa unyanyasaji. Na Balozi Haki za Binaadamu wa Mareakani huko Geneva ametoa wito wa kutolewa ripoti hiyo akisema ulimwengu unahitaji uhuru na ukweli wa hali halisi.
Soma zaidi:Bachelet akosolewa kwa ziara ya China
Awali Alhamis, Bachelet alithibitisha kupokea barua ambayo imesainiwa na takribani matraifa 40, na kuongeza haikuwa tayari kutoa majawabi ya sshinikizo la namna hiyo.
Chanzo: RTR