1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu anyooshea kidole utoaji mimba

LIONGO10 Mei 2007

Papa Benedicto wa 16 ametaka kuimarishwa kwa taasisi za kijamii, na ameshutumu tabia ya utoaji mimba.Kiongozi huyo wa kanisa la Katoliki duniani aliyasema hayo hapo jana katika ziara yake ya siku nne nchini Brazil.Wakati alikiwasili nchini Brazil hapo siku ya Jumatano, Papa Benedictor wa 16 alisema kuwa ziara yake hiyo itajikita zaidi katika masuala ya familia.

https://p.dw.com/p/CB4C
Baba mtakatifu akiwa na Rais Lula da Silva wa Brazil
Baba mtakatifu akiwa na Rais Lula da Silva wa BrazilPicha: AP

Kiongozi huyo mkuu wa kanisa katoliki duniani mwenye umri wa miaka 80 alisema kuwa hatoshindwa katika kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa msingi imara wa familia unaimarishwa.

Aidha ameshutumu utoaji mimba, akitolea mfano umuhimu wa kuhamasisha kuheshimu na kuthamini maisha toka pale mimba inapotungwa hadi kifo cha kawaida kinapotokea.

Karibu nusu ya waumini billioni 1.1 wa kanisa la katoliki duniani wako America ya Kusini, huku Brazil ikiwa na idadi kubwa.Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni kanisa hilo limekuwa likipoteza waumini wengi.

Asilimi 64 ya Wabrazil ni wakatoliki, lakini idadi hiyo imepungua sana katika moungo mmoja uliyopita, huku dini nyingine za kiinjili kutoka Marekani zikizidi kuimarika kwa asilimia 17.

Kanisa Katoliki pia lilipoteza mapambano muhimu nchini Mexico wakati jiji la Mexico lilipotangaza kuruhusu utoaji mimba.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleka Brazil, Baba Mtakatifu aliunga mkono tishio la maaskofu wa Mexico, kuwatenga wabunge wa jiji hilo waliyopitia sheria ya kuruhusu utoaji mimba.

Jiji la Mexico ni moja kati ya miji michache katika America ya Kusini ambapo utoaji mimba umeruhusiwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mimba hiyo

Papa Benedictor wa 16 muda mfupi ujayo anatarajiwa kuwahutubia vijana kiasi cha elfu 40 kutoka pembe zote za America ya Kusini waliyojazana katika uwanja wa mpira mjini Sao Paulo.

Baadaye atakuwa na mazungumzo na Rais wa Brazil nchi ambayo kwa sasa iko katika mjadala wa utoaji mimba.